Tuzo ya Hadithi Fupi ya Commonwealth inatolewa kwa hadithi bora ya Kiingereza ambayo haijawahi kuchapishwa (maneno 2,000 – 5,000). Hadithi zilizotungwa kwa lugha nyingine pia zinaweza kuwasilishwa. Kila mwaka, tunachagua washindi watano kutoka kanda tano za Commonwealth. Washindi wa kanda hutuzwa £2,500 na mshindi wa jumla hutuzwa £5,000. Kama hadithi iliyoshinda imetafsiriwa kwa Kiingereza, mtafsiri atapewa kiasi cha ziada.
Kujiunga na shindano ni bure.
Tungependa kuwaalika waandishi wanaoandika kwa Kiswahili, na ambao hawana mtafsiri wa Kiswahili, watume hadithi zao kwa Kiswahili. Kama sehemu ya tathmini yetu, hadithi hizo zitasomwa kwanza na wazoefu wa lugha ya Kiswahili. Hadithi yoyote itakayokubalika katika ngazi hii ya kwanza itatafsiriwa kwa Kiingereza na kusomwa na jopo la majaji katika ngazi ya kimataifa.
Tafadhali wasilisha hadithi yako kwa kupitia fomu inayopatikana kwa kubofya hapo chini.
[button link=”https://www.commonwealthwriters.org/submit-an-entry/”]INGIA KWENYE SHINDANO[/button]
Kwa maswali yoyote, tafadhali tuandikie writers@commonwealth.int.